Genesis 27:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yakobo akaingia ndani kwa baba yake, akamwita, “Baba!” Naye akaitika, “Naam! Ni nani wewe mwanangu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yakobo akaenda kwa baba yake, akasema, “Baba yangu.” Akajibu, “Naam, mwanangu. Wewe ni nani?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yakobo akaingia ndani kwa baba yake, akamwita, “Baba!” Naye akaitika, “Naam! Ni nani wewe mwanangu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.” Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.” Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yakobo akaingia ndani kwa baba yake, akamwita, “Baba!” Naye akaitika, “Naam! Ni nani wewe mwanangu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoingia mwa baba yake akasema: Baba! Naye akasema: Mimi hapa! Wewe ndiwe nani, mwanangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yakobo akaingia ndani kwa baba yake, akamwita: “Baba!” Naye akaitika: “Niko hapa! Ni nani wewe mwana wangu?”