Genesis 27:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, chukua silaha zako, yaani podo na upinde wako, uende porini ukaniwindie mnyama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa basi chukua silaha zako, podo na upinde, uende nyikani, ukaniwindie mawindo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, chukua silaha zako, yaani podo na upinde wako, uende porini ukaniwindie mnyama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upindi, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa ajili yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upinde, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa ajili yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, nakuomba, chukua uta wako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, chukua silaha zako, yaani podo na upinde wako, uende porini ukaniwindie mnyama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa yachukue mata yako, ndio podo lako na upindi wako, uende porini kuniwindia nyama!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, twaa silaha zako, maana yake podo na upinde wako, uende katika pori uniwindie nyama.