Genesis 27:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, naye Yakobo alipokuwa ndio tu ametoka mbele ya baba yake Isaka, Esau kaka yake Yakobo, akarudi kutoka mawindoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Isaka kumbariki Yakobo, na punde tu alipoondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, naye Yakobo alipokuwa ndio tu ametoka mbele ya baba yake Isaka, Esau kaka yake Yakobo, akarudi kutoka mawindoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Isaki kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Isaka kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na punde tu baada ya Yakobo kutoka mbele ya Isaka, babake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, naye Yakobo alipokuwa ndio tu ametoka mbele ya baba yake Isaka, Esau kaka yake Yakobo, akarudi kutoka mawindoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, naye Yakobo alipokwisha kutoka usoni pa baba yake Isaka, ndipo, kaka yake Esau aliporudi kwa kuwinda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Isaka alipokwisha kumubariki Yakobo, naye Yakobo alipokuwa angali tu anatoka mbele ya baba yake Isaka, Esau kaka ya Yakobo, akarudi kutoka katika mawindo.