Genesis 27:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Esau pia akatengeneza chakula kitamu, akampelekea baba yake, akamwambia, “Haya baba, inuka ule mawindo yangu mimi mwanao, ili upate kunibariki!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye pia akaandaa chakula kitamu, akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Esau pia akatengeneza chakula kitamu, akampelekea baba yake, akamwambia, “Haya baba, inuka ule mawindo yangu mimi mwanao, ili upate kunibariki!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye pia akaandaa chakula kitamu akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye pia akaandaa chakula kitamu akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake, Babangu na ainuke, ale mawindo ya mwanawe, ili aweze kunibariki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Esau pia akatengeneza chakula kitamu, akampelekea baba yake, akamwambia, “Haya baba, inuka ule mawindo yangu mimi mwanao, ili upate kunibariki!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akatengeneza kilaji cha urembo, akampelekea baba yake, akamwambia baba yake: Baba, inuka, ule nyama, mwanao alizokuwinda, roho yako ipate kunibariki!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Esau vilevile akatengeneza chakula kitamu, akamupelekea baba yake, akamwambia: “Basi baba, amuka ukule nyama ya mawindo yangu mimi mwana wako, upate kunibariki!”