Genesis 27:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Esau alipoyasikia maneno ya baba yake, akaangua kilio cha uchungu. Kisha akamwambia baba yake, “Ee baba yangu, nibariki na mimi, tafadhali!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia kwa sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki! Nibariki mimi pia, baba yangu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Esau alipoyasikia maneno ya baba yake, akaangua kilio cha uchungu. Kisha akamwambia baba yake, “Ee baba yangu, nibariki na mimi, tafadhali!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki mimi, mimi pia, baba yangu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki mimi, mimi pia, baba yangu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikuu na chenye uchungu mwingi sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Esau alipoyasikia maneno ya baba yake, akaangua kilio cha uchungu. Kisha akamwambia baba yake, “Ee baba yangu, nibariki na mimi, tafadhali!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Esau alipoyasikia haya maneno ya baba yake, akalia kilio kikubwa chenye uchungu mwingi sana, akamwambia baba yake: Baba, nibariki mimi nami!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Esau aliposikia maneno ya baba yake, akalia kilio kikubwa na cha uchungu. Kisha akamwambia baba yake: “Ee baba yangu, unibariki mimi, tafazali!”