Genesis 27:39 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Isaka, baba yake, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na ardhi yenye rutuba, na mbali na umande wa mbinguni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba yake Isaka akamjibu, “Makao yako yatakuwa mbali na utajiri wa dunia, mbali na umande wa mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Isaka, baba yake, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na ardhi yenye rutuba, na mbali na umande wa mbinguni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na utajiri wa dunia, mbali na umande wa mbinguni juu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baba yake Isaka akamjibu, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na utajiri wa dunia, mbali na umande wa mbinguni juu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia, Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako, Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Isaka, baba yake, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na ardhi yenye rutuba, na mbali na umande wa mbinguni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, baba yake Isaka alipomwitikia na kumwambia: Tazama! Hapo, utakapokaa, manono ya nchi yatakuwa mbali, nao umande wa mbinguni juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia, Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako, Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Isaka, baba yake, akamwambia: “Makao yako yatakuwa mbali na udongo wenye mboleo, na mbali na umande wa mbinguni.