Genesis 27:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Esau akamchukia Yakobo kwa sababu ya baraka aliyokuwa amepewa na baba yake. Esau akawaza, “Siku za matanga ya baba zitakapokwisha, ndipo nitakapomuua ndugu yangu Yakobo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia; ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Esau akamchukia Yakobo kwa sababu ya baraka aliyokuwa amepewa na baba yake. Esau akawaza, “Siku za matanga ya baba zitakapokwisha, ndipo nitakapomuua ndugu yangu Yakobo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia, ndipo nitamwua ndugu yangu Yakobo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia, ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ile baraka babaye aliyombariki. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Esau akamchukia Yakobo kwa sababu ya baraka aliyokuwa amepewa na baba yake. Esau akawaza, “Siku za matanga ya baba zitakapokwisha, ndipo nitakapomuua ndugu yangu Yakobo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Esau akamchukua Yakobo kwa ajili ya hiyo mbaraka, baba yake aliyombariki; kwa hiyo Esau akasema moyoni mwake: Siku za kumwombolezea baba ziko karibu; zitakapopita, nitamwua ndugu yangu Yakobo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Esau akamuchukia Yakobo kwa sababu ya baraka aliyokuwa amepewa na baba yake. Esau akawaza: “Siku za kilio cha baba zitakapokwisha, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.”