Genesis 27:45 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ghadhabu yake itakapopoa, naye atakapokuwa amesahau uliyomtendea, nitatuma mtu akurudishe. Kwa nini nifiwe na nyinyi wote wawili siku moja?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu yako atakapokuwa hana hasira nawe tena na amesahau uliyomtendea, nitakupelekea ujumbe urudi. Kwa nini niwapoteze nyote wawili siku moja?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapopeleka watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ghadhabu yake itakapopoa, naye atakapokuwa amesahau uliyomtendea, nitatuma mtu akurudishe. Kwa nini nifiwe na nyinyi wote wawili siku moja?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati ndugu yako atakapokuwa hana hasira nawe tena na amesahau uliyomtendea, nitakupelekea ujumbe urudi. Kwa nini niwapoteze wote wawili kwa siku moja?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati ndugu yako atakapokuwa hana hasira nawe tena na amesahau uliyomtendea, nitakupelekea ujumbe urudi. Kwa nini niwapoteze wote wawili kwa siku moja?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hadi ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapotuma watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ghadhabu yake itakapopoa, naye atakapokuwa amesahau uliyomtendea, nitatuma mtu akurudishe. Kwa nini nifiwe na nyinyi wote wawili siku moja?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, haya makali ya kaka yako yatakapotulia, aache kukuwazia mabaya kwa kuyasahau uliyomfanyizia, ndipo, nitakapotuma kukuchukua huko. Kwa nini mwataka, nifiwe nanyi wawili siku moja?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapopeleka watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kasirani yake itakapopoa juu yako, naye atakapokuwa amesahau mambo uliyomutendea, nitatuma mutu kwa kukutafuta kule. Kwa nini nikufiwe na ninyi wote wawili siku moja?”