Genesis 27:46 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Rebeka akamwambia Isaka, “Sina raha kabisa maishani kwa sababu ya hawa wanawake wa Esau Wahiti. Ikiwa Yakobo ataoa mmojawapo wa wanawake hawa Wahiti, maisha yangu yana faida gani?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Rebeka akamwambia Isaka, “Nimechukia maisha kwa sababu ya hawa wanawake Wahiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake Wahiti kama hawa, sitaona haja ya kuendelea kuishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidia nini?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Rebeka akamwambia Isaka, “Sina raha kabisa maishani kwa sababu ya hawa wanawake wa Esau Wahiti. Ikiwa Yakobo ataoa mmojawapo wa wanawake hawa Wahiti, maisha yangu yana faida gani?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Rebeka akamwambia Isaki, “Nimechukia kuishi kwa sababu ya hawa wanawake wa Kihiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake wa Kihiti kama hawa, sitakuwa na faida kuendelea kuishi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Rebeka akamwambia Isaka, “Nimechukia kuishi kwa sababu ya hawa wanawake wa Kihiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake wa Kihiti kama hawa, sitakuwa na faida kuendelea kuishi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidi nini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Rebeka akamwambia Isaka, “Sina raha kabisa maishani kwa sababu ya hawa wanawake wa Esau Wahiti. Ikiwa Yakobo ataoa mmojawapo wa wanawake hawa Wahiti, maisha yangu yana faida gani?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Rebeka akamwambia Isaka: Ninachukizwa sana na kuwapo kwangu kwa ajili ya hao wanawake wa Kihiti. Kama Yakobo naye ataoa mwanamke miongoni mwao vijana wa kike wa Kihiti walio hivyo, kama hawa walivyo miongoni mwa vijana wa nchi hii, mimi nimeletewa nini huku?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidia nini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Rebeka akamwambia Isaka: “Sina raha kabisa katika maisha kwa sababu ya hawa wanawake Wahiti wa Esau. Ikiwa Yakobo ataoa mumoja wa wanawake hawa Wahiti, maisha yangu yana faida gani?”