Genesis 27:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kumbe, wakati huo Isaka alipokuwa akiongea na Esau mwanawe, Rebeka alikuwa anasikiliza. Kwa hiyo, Esau alipokwenda porini kuwinda,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Rebeka alikuwa akisikiliza Isaka akizungumza na mwanawe Esau. Basi Esau alipoenda nyikani kuwinda mawindo ayalete,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kumbe, wakati huo Isaka alipokuwa akiongea na Esau mwanawe, Rebeka alikuwa anasikiliza. Kwa hiyo, Esau alipokwenda porini kuwinda,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaki alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaka alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kumbe, wakati huo Isaka alipokuwa akiongea na Esau mwanawe, Rebeka alikuwa anasikiliza. Kwa hiyo, Esau alipokwenda porini kuwinda,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Rebeka alikuwa ameyasikia, Isaka aliyomwambia mwanawe Esau. Esau alipokwisha kwenda porini kuwinda nyama ya kumpelekea baba,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kumbe, Rebeka alikuwa anasikiliza wakati ule Isaka alipokuwa akiongea na Esau, mwana wake. Kwa hiyo, Esau alipokwenda katika pori kuwinda,