Genesis 28:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yakobo akaamka asubuhi na mapema, akachukua lile jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake, akalisimika kama nguzo na kuliweka wakfu kwa kulimiminia mafuta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake asubuhi na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yakobo akaamka asubuhi na mapema, akachukua lile jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake, akalisimika kama nguzo na kuliweka wakfu kwa kulimiminia mafuta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asubuhi yake na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi yake na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yakobo akaamka asubuhi na mapema, akachukua lile jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake, akalisimika kama nguzo na kuliweka wakfu kwa kulimiminia mafuta.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asubuhi na mapema Yakobo akaamka, akalichukua lile jiwe, aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimika kuwa kielekezo, akalimiminia mafuta juu yake,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yakobo akaamuka asubui mapema, akatwaa lile jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake, akalisimika kama nguzo na kulitakasa kwa kulimiminia mafuta.