Genesis 28:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Esau alitambua kwamba Isaka alikuwa amembariki Yakobo na kumtuma aende kuoa huko Padan-aramu, na ya kuwa alipombariki, alimkataza asioe mwanamke Mkanaani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Esau akajua kuwa Isaka amembariki Yakobo na kumtuma Padan-Aramu ili achukue mke huko, na kwamba alipombariki alimwamuru, akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usitwae mke wa binti za Kanaani,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Esau alitambua kwamba Isaka alikuwa amembariki Yakobo na kumtuma aende kuoa huko Padan-aramu, na ya kuwa alipombariki, alimkataza asioe mwanamke Mkanaani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa Esau akajua kuwa Isaki amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Padan-Aramu ili achukue mke huko na kwamba alipombariki alimwamuru akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa Esau akajua kuwa Isaka amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Padan-Aramu ili achukue mke huko na kwamba alipombariki alimwamuru akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumtuma Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usioe mke wa binti za Kanaani,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Esau alitambua kwamba Isaka alikuwa amembariki Yakobo na kumtuma aende kuoa huko Padan-aramu, na ya kuwa alipombariki, alimkataza asioe mwanamke Mkanaani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Esau akaona, ya kuwa Isaka amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Mesopotamia, achukue mke huko, tena ya kuwa hapo alipombariki amemwagiza kwamba: Usijichukulie mke katika vijana wa kike wa Kanaani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usitwae mke wa binti za Kanaani,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Esau akatambua kwamba Isaka alibariki Yakobo na kumutuma aende kuoa kule Padani-Aramu, na kwamba alipomubariki, alimukataza asioe mwanamuke Mukanana.