Genesis 28:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, mbali na wale wake zake wengine, Esau akaenda kwa Ishmaeli, mwana wa Abrahamu, akamwoa Mahalathi binti Ishmaeli, dada yake Nebayothi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Esau akaenda kwa Ishmaeli, akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti ya Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Esau akaenda kwa Ishmaeli akamtwaa Mahalathi, binti Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, ndugu wa Nebayothi, kuwa mkewe pamoja na wakeze aliokuwa nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, mbali na wale wake zake wengine, Esau akaenda kwa Ishmaeli, mwana wa Abrahamu, akamwoa Mahalathi binti Ishmaeli, dada yake Nebayothi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ndipo akaenda kwa Ishmaeli akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti wa Ishmaeli mwana wa Abrahamu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Esau akaenda kwa Ishmaeli, akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti wa Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Esau akaenda kwa Ishmaeli akamtwaa Mahalathi, binti Ishmaeli mwana wa Abrahamu, ndugu wa Nebayothi, kuwa mkewe pamoja na wakeze aliokuwa nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, mbali na wale wake zake wengine, Esau akaenda kwa Ishmaeli, mwana wa Abrahamu, akamwoa Mahalathi binti Ishmaeli, dada yake Nebayothi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Esau alipokwenda kwa Isimaeli, akamchukua Mahalati, binti Isimaeli, mwana wa Aburahamu, umbu lake Nebayoti, kuwa mkewe pamoja na wakeze, aliokuwa nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Esau akaenda kwa Ishmaeli akamtwaa Mahalathi, binti Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, ndugu wa Nebayothi, kuwa mkewe pamoja na wakeze aliokuwa nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, Esau akakwenda kwa Isimaeli, mwana wa Abrahamu, akaoa Mahalati binti ya Isimaeli, dada ya Nebayoti.