Genesis 29:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yakobo alipomwona Raheli, bintiye Labani, kaka ya mama yake, na alipowaona kondoo wa Labani, mjomba wake, akaenda na kulivingirisha lile jiwe kwenye mdomo wa kisima, akalinywesha maji kundi la Labani, mjomba wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alienda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mamaye, na kondoo za Labani, ndugu wa mamaye, Yakobo akakaribia, na kulifingirisha lile jiwe litoke katika kinywa cha kisima, akawanywesha kondoo za Labani, ndugu wa mamaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yakobo alipomwona Raheli, bintiye Labani, kaka ya mama yake, na alipowaona kondoo wa Labani, mjomba wake, akaenda na kulivingirisha lile jiwe kwenye mdomo wa kisima, akalinywesha maji kundi la Labani, mjomba wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alikwenda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomoni mwa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alikwenda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomoni mwa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mamaye, na kondoo wa Labani, ndugu wa mamaye, Yakobo akakaribia, na kulibingirisha lile jiwe litoke katika kinywa cha kisima, akawanywesha kondoo wa Labani, ndugu wa mamaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yakobo alipomwona Raheli, bintiye Labani, kaka ya mama yake, na alipowaona kondoo wa Labani, mjomba wake, akaenda na kulivingirisha lile jiwe kwenye mdomo wa kisima, akalinywesha maji kundi la Labani, mjomba wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yakobo alipomwona Raheli, binti Labani aliyekuwa umbu la mama yake, nalo kundi la Labani aliyekuwa umbu la mama yake, Yakobo akafika karibu, akalifingirisha lile jiwe, liondoke mdomoni pa kisima, akawanywesha mbuzi na kondoo wa Labani aliyekuwa umbu la mama yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mamaye, na kondoo za Labani, ndugu wa mamaye, Yakobo akakaribia, na kulifingirisha lile jiwe litoke katika kinywa cha kisima, akawanywesha kondoo za Labani, ndugu wa mamaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yakobo akamwona Rakeli, binti ya mujomba wake Labani. Akaona kondoo ambao vilevile ni wa mujomba wake. Akakwenda na kuliviringisha lile jiwe kwenye mudomo wa kisima. Akakunywesha maji kundi la mujomba wake.