Genesis 29:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Labani aliposikia habari za Yakobo, mpwa wake, alikwenda mbio kumlaki, akamkumbatia, akambusu, akamkaribisha nyumbani kwake. Yakobo akamsimulia Labani mambo yote yaliyotokea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu, halafu akamleta nyumbani mwake, naye Yakobo akamwambia mambo hayo yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Labani aliposikia habari za Yakobo, mpwa wake, alikwenda mbio kumlaki, akamkumbatia, akambusu, akamkaribisha nyumbani kwake. Yakobo akamsimulia Labani mambo yote yaliyotokea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu halafu akamleta nyumbani kwake, kisha Yakobo akamwambia mambo yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu, halafu akamleta nyumbani kwake, kisha Yakobo akamwambia mambo yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Labani aliposikia habari za Yakobo, mpwa wake, alikwenda mbio kumlaki, akamkumbatia, akambusu, akamkaribisha nyumbani kwake. Yakobo akamsimulia Labani mambo yote yaliyotokea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Labani alipozisikia habari za Yakobo, mwana wa umbu lake, akamkimbilia, akamkumbatia na kumnonea, kisha akampeleka nyumbani mwake. Naye akamsimulia Labani hayo mambo yote ya kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Labani aliposikia habari za mwipwa wake Yakobo, alikwenda mbio kumupokea, akamukumbatia, akamubusu, akamukaribisha ndani ya nyumba yake. Yakobo akamwelezea Labani mambo yote yaliyotokea.