Genesis 29:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja Labani alimwambia Yakobo, “Wewe ni jamaa yangu lakini hiyo haimaanishi kwamba utanitumikia bure. Niambie unataka ujira kiasi gani!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Labani akamwambia, “Kwa vile wewe ni jamaa yangu, ndiyo sababu unifanyie kazi bila ujira? Niambie ujira wako utakuwa nini.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja Labani alimwambia Yakobo, “Wewe ni jamaa yangu lakini hiyo haimaanishi kwamba utanitumikia bure. Niambie unataka ujira kiasi gani!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Labani akamwambia, “Kwa vile wewe ni jamaa yangu, ndiyo unifanyie kazi bila ujira? Niambie ujira wako utakuwa nini.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Labani akamwambia, “Kwa vile wewe ni jamaa yangu, ndiyo sababu unifanyie kazi bila ujira? Niambie ujira wako utakuwa nini.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni jamaa yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja Labani alimwambia Yakobo, “Wewe ni jamaa yangu lakini hiyo haimaanishi kwamba utanitumikia bure. Niambie unataka ujira kiasi gani!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Labani akamwambia Yakobo: Ijapo u ndugu yangu, kwa hiyo utanitumikia bure? Niambie mshahara wako, unaoutaka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja Labani akamwambia Yakobo: “Wewe ni jamaa yangu lakini hiyo haisemi kwamba utanitumikia bure. Uniambie unataka mushahara gani!”