Genesis 29:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kawaida, makundi yote ya kondoo yalipokusanyika, wachungaji walivingirisha hilo jiwe kwa pamoja toka kisimani na kuwanywesha kondoo. Halafu walikifunika tena kisima kwa jiwe hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kondoo walipokusanyika hapo, wachungaji walilivingirisha jiwe hilo kutoka mdomo wa kisima. Kisha walilirudisha jiwe mahali pake juu ya mdomo wa kisima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Makundi yote hukusanyika huko, watu wakafingirisha hilo jiwe katika kinywa cha kisima wakawanywesha kondoo, na kulirudisha jiwe juu ya kinywa cha kisima mahali pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kawaida, makundi yote ya kondoo yalipokusanyika, wachungaji walivingirisha hilo jiwe kwa pamoja toka kisimani na kuwanywesha kondoo. Halafu walikifunika tena kisima kwa jiwe hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati kondoo wanapokuwa wamekusanyika hapo, wachungaji huvingirisha jiwe hilo kutoka kwenye mdomo wa kisima na kunywesha kondoo. Kisha hulirudisha jiwe mahali pake juu ya mdomo wa kisima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati kondoo wanapokuwa wamekusanyika hapo, wachungaji huvingirisha jiwe hilo kutoka kwenye mdomo wa kisima na kunywesha kondoo. Kisha hulirudisha jiwe mahali pake juu ya mdomo wa kisima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makundi yote hukusanyika huko, watu wakabingirisha hilo jiwe katika kinywa cha kisima wakawanywesha kondoo, na kulirudisha jiwe juu ya kinywa cha kisima mahali pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kawaida, makundi yote ya kondoo yalipokusanyika, wachungaji walivingirisha hilo jiwe kwa pamoja toka kisimani na kuwanywesha kondoo. Halafu walikifunika tena kisima kwa jiwe hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko ndiko, makundi yote yalikokusanyikia, kisha wakaliondoa hilo jiwe mdomoni pa kisima na kulifingirisha; tena walipokwisha kuyanywesha makundi yao, wakalirudisha mahali pake mdomoni pa kisima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Makundi yote hukusanyika huko, watu wakafingirisha hilo jiwe katika kinywa cha kisima wakawanywesha kondoo, na kulirudisha jiwe juu ya kinywa cha kisima mahali pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa kawaida, makundi yote ya kondoo yalipokusanyika, wachungaji walirudisha lile jiwe kwa pamoja toka kwenye kisima na kuwakunywesha kondoo. Halafu walifunika tena kisima kwa jiwe lile.