Genesis 29:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Simeoni, akisema, “Mwenyezi-Mungu amenipa mtoto mwingine wa kiume kwa sababu amesikia jinsi ninavyochukiwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita jina Simeoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Simeoni, akisema, “Mwenyezi-Mungu amenipa mtoto mwingine wa kiume kwa sababu amesikia jinsi ninavyochukiwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Kwa sababu BWANA alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita Simeoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Kwa sababu bwana alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita Simeoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Simeoni, akisema, “Mwenyezi-Mungu amenipa mtoto mwingine wa kiume kwa sababu amesikia jinsi ninavyochukiwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akapata mimba tena, akazaa mtoto mume, akasema: Kwa kuwa Bwana amesikia, ya kama nimechukiwa, amenipa huyu mtoto naye, kwa hiyo akamwita jina lake Simeoni (Kusikiwa).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lea akapata mimba tena, akazaa mutoto mwanaume, akamwita Simeoni, akisema: “Yawe amenipa mutoto mwingine mwanaume kwa sababu amesikia jinsi ninavyochukiwa.”