Genesis 29:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akapata mimba mara nyingine, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Lawi, akisema, “Wakati huu mume wangu atajiunga nami, kwani nimemzalia watoto watatu wa kiume.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Sasa mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita jina Lawi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akapata mimba mara nyingine, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Lawi, akisema, “Wakati huu mume wangu atajiunga nami, kwani nimemzalia watoto watatu wa kiume.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Sasa afadhali mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita Lawi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Sasa afadhali mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita Lawi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akapata mimba mara nyingine, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Lawi, akisema, “Wakati huu mume wangu atajiunga nami, kwani nimemzalia watoto watatu wa kiume.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akapata mimba tena, akazaa mtoto mume, akasema: Sasa mara hii mume wangu ataandamanishwa na mimi, kwa kuwa nimemzalia watoto waume watatu, kwa hiyo akamwita jina lake Lawi (Mwandamano).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akapata mimba mara nyingine, akazaa mutoto mwanaume, akamwita Lawi, akisema: “Wakati huu mume wangu atajiunga nami, maana nimemuzalia watoto watatu wanaume.”