Genesis 29:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Yuda, akisema, “Safari hii nitamsifu Mwenyezi-Mungu.” Kisha Lea akaacha kuzaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Wakati huu nitamsifu Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo akamwita jina Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Yuda, akisema, “Safari hii nitamsifu Mwenyezi-Mungu.” Kisha Lea akaacha kuzaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifu BWANA.” Kwa hiyo akamwita Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifu bwana.” Kwa hiyo akamwita Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lea akapata mimba tena, akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Yuda, akisema, “Safari hii nitamsifu Mwenyezi-Mungu.” Kisha Lea akaacha kuzaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akapata mimba tena, akazaa mtoto mume, akasema: Mara hii nitamshukuru Bwana, kwa hiyo akamwita jina lake Yuda (Shukrani). Kisha akakoma kuzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lea akapata mimba tena, akazaa mutoto mwanaume, akamwita Yuda, akisema: “Mara hii nitamusifu Yawe.” Kisha Lea akaacha kuzaa.