Genesis 29:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Yakobo akawaambia, “Naona bado ni mchana, na si wakati wa kuwakusanya kondoo pamoja. Basi, wanywesheni kondoo maji, mwende mkawachunge.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia, “Tazama, jua bado liko juu, si wakati wa kukusanya mifugo. Nywesheni kondoo na mwarudishe malishoni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Tazama, ukali mchana bado, wala sio wakati wa kukusanya wanyama; wanywesheni kondoo, mwende kuwalisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Yakobo akawaambia, “Naona bado ni mchana, na si wakati wa kuwakusanya kondoo pamoja. Basi, wanywesheni kondoo maji, mwende mkawachunge.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Tazama, jua bado liko juu, si wakati wa kukusanya kondoo. Nywesheni kondoo na mwarudishe malishoni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema, “Tazama, jua bado liko juu, si wakati wa kukusanya mifugo. Nywesheni kondoo na mwarudishe malishoni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Tazama, kungali mchana bado, wala sio wakati wa kukusanya wanyama; wanywesheni kondoo, mwende kuwalisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Yakobo akawaambia, “Naona bado ni mchana, na si wakati wa kuwakusanya kondoo pamoja. Basi, wanywesheni kondoo maji, mwende mkawachunge.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Tazameni, jua liko juu bado, saa za kukusanyikia makundi hazijatimia bado; wanywesheni mbuzi na kondoo, kisha walisheni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Tazama, ukali mchana bado, wala sio wakati wa kukusanya wanyama; wanywesheni kondoo, mwende kuwalisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yakobo akawaambia: “Ninaona ingaliki muchana, na si wakati wa kuwakusanya kondoo pamoja. Basi, mukunyweshe kondoo maji, muende kuwachunga.”