Genesis 3:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini walioumbwa na Mwenyezi-Mungu. Basi, nyoka akamwambia huyo mwanamke, “Ati Mungu alisema msile matunda ya mti wowote bustanini?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi nyoka alikuwa mjanja kuliko wanyama pori wote ambao Bwana Mwenyezi Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini walioumbwa na Mwenyezi-Mungu. Basi, nyoka akamwambia huyo mwanamke, “Ati Mungu alisema msile matunda ya mti wowote bustanini?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao BWANA Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wo wote wa bustanini’?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao bwana Mwenyezi Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini walioumbwa na Mwenyezi-Mungu. Basi, nyoka akamwambia huyo mwanamke, “Ati Mungu alisema msile matunda ya mti wowote bustanini?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyoka alikuwa mjanja kuliko nyama wote wa porini, Bwana Mungu aliowafanya. Naye akamwambia mwanamke: Kumbe Mungu amewakataza kuila miti yote iliyomo humu shambani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyoka alikuwa mwerevu kuliko nyama wote wa pori walioumbwa na Yawe Mungu. Basi, nyoka akamwambia yule mwanamuke: “Ni kweli Mungu alisema musikule matunda ya muti wowote katika bustani?”