Genesis 3:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa, binadamu amekuwa kama mmoja wetu, anajua mema na mabaya. Lazima kumzuia kula lile tunda la mti wa uhai, kwani akilila ataishi milele!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Bwana Mwenyezi Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa, binadamu amekuwa kama mmoja wetu, anajua mema na mabaya. Lazima kumzuia kula lile tunda la mti wa uhai, kwani akilila ataishi milele!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyosha mkono wake na kuchuma pia kutoka katika mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana Mwenyezi Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa, binadamu amekuwa kama mmoja wetu, anajua mema na mabaya. Lazima kumzuia kula lile tunda la mti wa uhai, kwani akilila ataishi milele!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Bwana Mungu akasema: Ninamwona Adamu, ya kuwa amekwisha kuwa kama mwenzetu kwa kujua mema na mabaya; labda sasa ataupeleka mkono wake, achume nayo matunda ya mti wa uzima na kuyala, apate kuwapo kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yawe Mungu akasema: “Sasa, mwanadamu amekuwa kama mumoja wetu, anajua mazuri na mabaya. Inafaa kumuzuia kula lile tunda la muti wa uzima, maana akilikula ataishi milele.”