Genesis 3:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jioni, wakati wa kupunga upepo, huyo mwanamume na mkewe wakasikia hatua za Mwenyezi-Mungu akitembea bustanini, nao wakajificha kati ya miti ya bustani, Mwenyezi-Mungu asipate kuwaona.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa Bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jioni, wakati wa kupunga upepo, huyo mwanamume na mkewe wakasikia hatua za Mwenyezi-Mungu akitembea bustanini, nao wakajificha kati ya miti ya bustani, Mwenyezi-Mungu asipate kuwaona.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya BWANA Mungu alipokuwa akitembea bustanini wakati wa utulivu wa jioni, wakajificha kutoka mbele za BWANA Mungu katikati ya miti ya bustani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya bwana Mwenyezi Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jioni, wakati wa kupunga upepo, huyo mwanamume na mkewe wakasikia hatua za Mwenyezi-Mungu akitembea bustanini, nao wakajificha kati ya miti ya bustani, Mwenyezi-Mungu asipate kuwaona.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jua lilipokuwa limeponga, wakakisikia kishindo cha Bwana Mungu, akitembea shambani; ndipo, Adamu na mkewe walipojificha kwenye miti ya shamba, Bwana Mungu asiwaone.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Magaribi mwanaume na muke wake wakasikia Yawe Mungu akitembea katika bustani, nao wakajificha kati ya miti ya bustani, Yawe Mungu asipate kuwaona.