Genesis 30:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikawa wakati wa mavuno ya ngano, Reubeni alikwenda shambani na huko akapata tunguja, akamletea mama yake Lea. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali, nipe baadhi ya tunguja za mwanao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msimu wa kuvuna ngano, Reubeni akaenda shambani akachuma tunguja ambazo alizileta kwa Lea mama yake. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali nakuomba unipe baadhi ya tunguja za mwanao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikawa wakati wa mavuno ya ngano, Reubeni alikwenda shambani na huko akapata tunguja, akamletea mama yake Lea. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali, nipe baadhi ya tunguja za mwanao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa kuvuna ngano, Reubeni akaenda shambani akakuta tunguja, ambazo alizileta kwa Lea mama yake. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali nakuomba unipe baadhi ya tunguja za mwanao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa kuvuna ngano, Reubeni akaenda shambani akakuta tunguja, ambazo alizileta kwa Lea mama yake. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali nakuomba unipe baadhi ya tunguja za mwanao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja shambani, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikawa wakati wa mavuno ya ngano, Reubeni alikwenda shambani na huko akapata tunguja, akamletea mama yake Lea. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali, nipe baadhi ya tunguja za mwanao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Rubeni alipotembea siku za mavuno ya ngano, akaona tunguja shambani akampelekea mama yake. Naye Raheli akamwambia Lea: Unigawie na mimi tunguja za mwanao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikakuwa wakati wa mavuno ya ngano, Rubeni alikwenda kwenye shamba na kule akapata matunda ya dudai, akamuletea mama yake Lea. Rakeli akamwambia Lea: “Tafazali, unipe sehemu ya dudai za mwana wako.”