Genesis 30:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Raheli akamjibu, “Mjakazi wangu Bilha yupo. Lala naye ili azae watoto badala yangu, nami pia nipate watoto kutokana naye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mjakazi wangu. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto, na kupitia kwake mimi pia niweze kuwa na uzao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae juu ya magoti yangu, nami nipate uzao kwa yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Raheli akamjibu, “Mjakazi wangu Bilha yupo. Lala naye ili azae watoto badala yangu, nami pia nipate watoto kutokana naye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mtumishi wangu wa kike. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto na kwa kupitia yeye mimi pia niweze kuwa na uzao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mtumishi wangu wa kike. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto na kwa kupitia yeye mimi pia niweze kuwa na uzao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae kwa niaba yangu, nami nipate uzao kwa yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Raheli akamjibu, “Mjakazi wangu Bilha yupo. Lala naye ili azae watoto badala yangu, nami pia nipate watoto kutokana naye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akajibu: Tazama! Yuko kijakazi wangu Biliha, ingia kwake, azae magotini pangu, mimi nami nipate mlango kwake yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae juu ya magoti yangu, nami nipate uzao kwa yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Rakeli akamujibu: “Mujakazi wangu Biliha yuko. Lala naye kusudi azae watoto pahali pangu, nami vilevile nipate watoto kutokana naye.”