Genesis 31:34 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Raheli alikuwa amevichukua hivyo vinyago, akavificha chini ya matandiko ya ngamia na kuketi juu yake. Labani akavitafuta katika hema lote; lakini hakuvipata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Raheli ndiye alikuwa ameichukua ile miungu ya nyumbani mwao na kuiweka katika matandiko ya ngamia, na kukalia. Labani akatafuta kila mahali kwenye hema lakini hakupata chochote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Raheli alikuwa amevitwaa vile vinyago ameviweka katika matandiko ya ngamia, na kuvikalia. Labani akapapasa hema yote wala hakuviona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Raheli alikuwa amevichukua hivyo vinyago, akavificha chini ya matandiko ya ngamia na kuketi juu yake. Labani akavitafuta katika hema lote; lakini hakuvipata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Raheli ndiye aliyekuwa amechukua ile miungu ya nyumbani kwao na kuiweka katika matandiko ya ngamia na kukalia. Labani akatafuta kila mahali kwenye hema lakini hakupata cho chote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Raheli ndiye alikuwa amechukua ile miungu ya nyumbani kwao na kuiweka katika matandiko ya ngamia na kukalia. Labani akatafuta kila mahali kwenye hema lakini hakupata chochote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Raheli alikuwa amevitwaa vile vinyago ameviweka katika matandiko ya ngamia, na kuvikalia. Labani akapapasa hema yote wala hakuviona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Raheli alikuwa amevichukua hivyo vinyago, akavificha chini ya matandiko ya ngamia na kuketi juu yake. Labani akavitafuta katika hema lote; lakini hakuvipata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Raheli alikuwa amevificha vinyago vya nyumbani ndani ya matandiko ya ngamia, akayakalia. Naye Labani alipoyapapasapapasa yote yaliyomo hemani hakuona kitu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Raheli alikuwa amevitwaa vile vinyago ameviweka katika matandiko ya ngamia, na kuvikalia. Labani akapapasa hema yote wala hakuviona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Rakeli alikuwa ametwaa zile sanamu, akazificha chini ya matandiko ya ngamia na kuketi juu yake. Labani akazitafuta katika hema lote; lakini hakuzipata.