Genesis 31:35 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Raheli akamwambia baba yake, “Samahani baba, usiudhike, kwani siwezi kusimama mbele yako kwa sababu nimo katika siku zangu.” Basi, Labani akavitafuta vinyago vya miungu yake, lakini hakuvipata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Raheli akamwambia baba yake, “Usikasirike bwana wangu, kwa kuwa siwezi kusimama ukiwepo, niko katika hedhi.” Labani akatafuta lakini hakuweza kuipata miungu ya nyumbani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Raheli akamwambia baba yake, “Samahani baba, usiudhike, kwani siwezi kusimama mbele yako kwa sababu nimo katika siku zangu.” Basi, Labani akavitafuta vinyago vya miungu yake, lakini hakuvipata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Raheli akamwambia baba yake, “Usikasirike, bwana wangu kwa kuwa siwezi kusimama ukiwepo, niko katika hedhi.” Labani akatafuta lakini hakuweza kuipata miungu ya nyumbani kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Raheli akamwambia baba yake, “Usikasirike, bwana wangu kwa kuwa siwezi kusimama ukiwepo, niko katika hedhi.” Labani akatafuta lakini hakuweza kuipata miungu ya nyumbani kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Raheli akamwambia baba yake, “Samahani baba, usiudhike, kwani siwezi kusimama mbele yako kwa sababu nimo katika siku zangu.” Basi, Labani akavitafuta vinyago vya miungu yake, lakini hakuvipata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Raheli akamwambia baba yake: Usikasirike, bwana wangu! Kwani siwezi kuinuka mbele yako, kwani mambo yetu ya kike yamenipata. Kwa hiyo hakuviona vile vinyago vya nyumbani, ijapo alivitafuta po pote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Rakeli akamwambia baba yake: “Tafazali baba, usiuzike, maana siwezi kusimama mbele yako kwa sababu niko katika siku zangu.” Basi, Labani akatafuta sanamu za miungu yake, lakini hakuzipata.