Genesis 31:37 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, umepata nini kilicho chako hata baada ya kuipekua mizigo yangu yote? Kiweke mbele ya ndugu zangu na ndugu zako, ili wao waamue kati yetu sisi wawili!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa kwa kuwa umepekua vitu vyangu vyote, umepata nini kilicho cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya jamaa yako na yangu, nao waamue kati yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, umepata nini kilicho chako hata baada ya kuipekua mizigo yangu yote? Kiweke mbele ya ndugu zangu na ndugu zako, ili wao waamue kati yetu sisi wawili!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa kwa kuwa umepekua vitu vyangu vyote umepata nini kilicho cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya jamaa yako na yangu, nao waamue kati yetu sisi wawili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa kwa kuwa umepekua vitu vyangu vyote umepata nini kilicho cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya jamaa yako na yangu, nao waamue kati yetu sisi wawili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umepekua vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, umepata nini kilicho chako hata baada ya kuipekua mizigo yangu yote? Kiweke mbele ya ndugu zangu na ndugu zako, ili wao waamue kati yetu sisi wawili!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umevipapasapapasa vyombo vyangu vyote pia, lakini umeona kitu gani kilicho cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu walio na ndugu zako, watuamue sisi wawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umepata kitu gani kinachokuwa chako hata kupekua mizigo yangu yote? Ukiweke mbele ya wandugu zangu na wandugu zako, kusudi wao waamue kati yetu sisi wawili!