Genesis 31:39 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi sikukuletea hata mara moja mnyama wako aliyeuawa na mnyama wa porini, bali nilifidia hasara hiyo mimi mwenyewe. Wewe ulinitaka nilipe bila kujali kama aliibiwa mchana au usiku!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sijakuletea mfugo aliyeraruliwa na wanyama pori, bali nimegharimia hasara mwenyewe. Tena umenidai malipo kwa chochote kilichoibwa mchana au usiku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi sikukuletea hata mara moja mnyama wako aliyeuawa na mnyama wa porini, bali nilifidia hasara hiyo mimi mwenyewe. Wewe ulinitaka nilipe bila kujali kama aliibiwa mchana au usiku!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikukuletea mfugo aliyeraruliwa na wanyama pori, nilibeba hasara mimi mwenyewe. Tena ulinidai malipo kwa cho chote kilichoibwa mchana au usiku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikukuletea mfugo aliyeraruliwa na wanyama pori, nilibeba hasara mimi mwenyewe. Tena ulinidai malipo kwa chochote kilichoibwa mchana au usiku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kilichoraruliwa na mnyama wa porini sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, kiwe kilichukuliwa mchana au kilichukuliwa usiku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi sikukuletea hata mara moja mnyama wako aliyeuawa na mnyama wa porini, bali nilifidia hasara hiyo mimi mwenyewe. Wewe ulinitaka nilipe bila kujali kama aliibiwa mchana au usiku!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walioraruliwa na nyama sikukupelekea, sikuwa na budi kuwalipa, ukawataka mikononi mwangu nao walioibiwa mchana, nao walioibiwa usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi sikukuletea nyama wako aliyeuawa na nyama wa pori, lakini nilibeba hasara hiyo mimi mwenyewe. Wewe ulinidai nyama aliyeibwa muchana au usiku!