Genesis 31:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi Yakobo akataka Raheli na Lea waitwe; nao wakamwendea mbugani alikokuwa anachunga wanyama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Yakobo akatuma ujumbe kwa Raheli na Lea waje malishoni kwenye makundi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yakobo akatuma watu, akawaita Raheli na Lea waje nyikani kwenye wanyama wake. Akawaambia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi Yakobo akataka Raheli na Lea waitwe; nao wakamwendea mbugani alikokuwa anachunga wanyama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Yakobo akatuma ujumbe kwa Raheli na Lea waje machungani yalikokuwa makundi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Yakobo akatuma ujumbe kwa Raheli na Lea waje machungani yalikokuwa makundi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yakobo akatuma watu ili kuwaita Raheli na Lea waje malishoni kwenye mifugo wake. Akawaambia,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi Yakobo akataka Raheli na Lea waitwe; nao wakamwendea mbugani alikokuwa anachunga wanyama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yakobo alipotuma kumwita Raheli naye Lea, waje porini kwake kwenye mbuzi na kondoo wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yakobo akatuma watu, akawaita Raheli na Lea waje nyikani kwenye wanyama wake. Akawaambia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Yakobo akatuma watu kuita Rakeli na Lea kumukutana katika shamba alimokuwa anachunga nyama wake.