Genesis 31:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa miaka ishirini hii yote nimeishi nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka kumi na minne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita nikawachunga wanyama wako. Lakini wewe, ukabadilisha ujira wangu mara kumi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Imekuwa hivi kwa miaka ile ishirini niliyokuwa nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka ile kumi na nne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita kwa ajili ya makundi yako, nawe ulibadilisha ujira wangu mara kumi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa miaka ishirini hii yote nimeishi nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka kumi na minne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita nikawachunga wanyama wako. Lakini wewe, ukabadilisha ujira wangu mara kumi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilikuwa hivi kwa miaka ile ishirini niliyokuwa nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka ile kumi na minne kwa ajili ya binti zako wawili, miaka sita kwa ajili ya makundi yako, nawe ulibadilisha ujira wangu mara kumi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilikuwa hivi kwa miaka ile ishirini niliyokuwa nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka ile kumi na minne kwa ajili ya binti zako wawili, miaka sita kwa ajili ya makundi yako, nawe ulibadilisha ujira wangu mara kumi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa miaka ishirini hii yote nimeishi nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka kumi na minne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita nikawachunga wanyama wako. Lakini wewe, ukabadilisha ujira wangu mara kumi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo ndivyo, nilivyokutumikia nyumbani mwako miaka hii 20, miaka kumi na minne, niwapate hawa wano wawili wa kike, tena miaka sita, niyapate haya makundi yako, nawe umeugeuza mshahara wangu mara kumi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa miaka makumi mbili hii yote nimeishi katika nyumba yako. Nilikutumikia miaka kumi na mine kwa ajili ya wabinti zako wawili, na miaka sita nikachunga nyama wako. Lakini wewe, ukabadilisha mushahara wangu mara kumi.