Genesis 33:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yakobo akamwambia, “La! Kama kweli umekubali kunipokea, basi, nakusihi uipokee zawadi yangu. Hakika, kuuona uso wako ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa vile ulivyonipokea kwa wema mkubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yakobo akasema, “La hasha! Tafadhali, kama nimepata kibali machoni pako, upokee zawadi hii kutoka kwangu. Kwa maana kuuona uso wako ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa kuwa umenipokea kwa kibali kikubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yakobo akasema, Sivyo; kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, iwapo nimeona uso wako kama kuona uso wa Mungu, ukapendezwa nami.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yakobo akamwambia, “La! Kama kweli umekubali kunipokea, basi, nakusihi uipokee zawadi yangu. Hakika, kuuona uso wako ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa vile ulivyonipokea kwa wema mkubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yakobo akasema, “La hasha! Tafadhali, kama nimepata kibali machoni pako, upokee zawadi hii kutoka kwangu. Kwa maana kuuona uso wako, ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa kuwa umenipokea kwa takabali kubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yakobo akasema, “La hasha! Tafadhali, kama nimepata kibali machoni pako, upokee zawadi hii kutoka kwangu. Kwa maana kuuona uso wako, ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa kuwa umenipokea kwa takabali kubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yakobo akasema, Sivyo; nakuomba kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, iwapo nimeona uso wako kama kuuona uso wa Mungu, ukapendezwa nami.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yakobo akamwambia, “La! Kama kweli umekubali kunipokea, basi, nakusihi uipokee zawadi yangu. Hakika, kuuona uso wako ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa vile ulivyonipokea kwa wema mkubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Yakobo akajibu: Sivyo! Kama nimeona upendeleo machoni pako, yachukue matunzo haya mkononi mwangu! Kwa kuwa nilipouona uso wako, ikawa, kama nimeuona uso wake Mungu, maana umenipokea na kupendezwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yakobo akasema, Sivyo; kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, iwapo nimeona uso wako kama kuona uso wa Mungu, ukapendezwa nami.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yakobo akamwambia: “Hapana! Kama kweli nimekubaliwa mbele yako, ninakusihi uipokee zawadi yangu. Hakika, kuona uso wako ni kama kuona uso wa Mungu, kwa vile ulivyonipokea kwa wema mukubwa.