Genesis 33:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu, wewe unajua kwamba watoto hawa ni wachanga, na kwamba mifugo hii inanyonyesha, nami sina budi kuitunza; kama wanyama hawa watapelekwa mbio kwa siku moja, wote watakufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu, unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa ng’ombe na kondoo wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng'ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu, wewe unajua kwamba watoto hawa ni wachanga, na kwamba mifugo hii inanyonyesha, nami sina budi kuitunza; kama wanyama hawa watapelekwa mbio kwa siku moja, wote watakufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa kondoo wake na ng'ombe wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa kondoo wake na ng’ombe wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng'ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu, wewe unajua kwamba watoto hawa ni wachanga, na kwamba mifugo hii inanyonyesha, nami sina budi kuitunza; kama wanyama hawa watapelekwa mbio kwa siku moja, wote watakufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Yakobo akamwambia: Bwana wangu anajua, ya kuwa watoto hawa ni wachanga bado, tena ninao mbuzi na kondoo na ng'ombe wenye kunyonyesha, wao wakikimbizwa kwenda zaidi siku moja tu, kundi lote litakufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng’ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yakobo akamwambia: “Bwana wangu, wewe unajua kwamba watoto hawa ni wachanga, na kwamba nyama hawa wananyonyesha, nami ninapaswa kuwatunza. Kama nyama hawa watapelekwa mbio kwa siku moja, wote watakufa.