Genesis 33:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Esau akauliza, “Nini maana ya kundi hili nililokutana nalo njiani?” Yakobo akamjibu, “Nilitumaini kupata fadhili kwako ee bwana wangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Esau akauliza, “Makundi hayo yote niliyokutana nayo yana maana gani?” Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Kundi hili lote nililolikuta, maana yake ni nini? Akasema, Kunipatia kibali machoni pa bwana wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Esau akauliza, “Nini maana ya kundi hili nililokutana nalo njiani?” Yakobo akamjibu, “Nilitumaini kupata fadhili kwako ee bwana wangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Esau akauliza, “Una maana gani kuhusu makundi hayo yote niliyokutana nayo?” Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Esau akauliza, “Una maana gani kuhusu makundi hayo yote niliyokutana nayo?” Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Kundi hili lote nililokutana nalo, maana yake ni nini? Akasema, Ili kunipatia kibali machoni pa bwana wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Esau akauliza, “Nini maana ya kundi hili nililokutana nalo njiani?” Yakobo akamjibu, “Nilitumaini kupata fadhili kwako ee bwana wangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akauliza tena: Hicho kikosi chako chote, nilichokutana nacho, ni cha nini? Akasema: Ni kwamba, nijipatie upendeleo machoni pa bwana wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Kundi hili lote nililolikuta, maana yake ni nini? Akasema, Kunipatia kibali machoni pa bwana wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Esau akauliza: “Kundi lile nililokutana nalo katika njia lina maana gani?” Yakobo akamujibu: “Nilitumaini kupata kukubaliwa mbele yako, ee bwana wangu.”