Genesis 34:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu hawa ni marafiki zetu. Tuwakaribishe waishi nchini mwetu na kufanya biashara, kwa sababu tunayo nchi ya kututosha sisi na wao pia; kisha tutaoa binti zao na kuwaoza binti zetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakasema, “Hawa wanaume ni rafiki zetu. Tuwaruhusu waishi katika nchi yetu na kufanya biashara ndani yake; nchi ina nafasi tele kwa ajili yao. Tunaweza kuoa binti zao, nao wanaweza kuoa binti zetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu hawa wana amani nasi, basi na wakae katika nchi, na kufanya biashara humo; kwa maana nchi ni kubwa, yawatosha; na tuwatwae binti zao kuwa wake zetu, na binti zetu tuwape wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu hawa ni marafiki zetu. Tuwakaribishe waishi nchini mwetu na kufanya biashara, kwa sababu tunayo nchi ya kututosha sisi na wao pia; kisha tutaoa binti zao na kuwaoza binti zetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakasema, “Hawa watu ni marafiki kwetu, tuwaruhusu waishi katika nchi yetu na kufanya biashara ndani yake, nchi ina nafasi tele kwa ajili yao. Tunaweza kuoa binti zao. Nao wanaweza kuoa binti zetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakasema, “Hawa watu ni marafiki kwetu, tuwaruhusu waishi katika nchi yetu na kufanya biashara ndani yake, nchi ina nafasi tele kwa ajili yao. Tunaweza kuoa binti zao. Nao wanaweza kuoa binti zetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu hawa wana amani nasi, basi na wakae katika nchi, na kufanya biashara humo; kwa maana nchi ni kubwa, yawatosha; na tuwatwae binti zao kuwa wake zetu, na binti zetu tuwape wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu hawa ni marafiki zetu. Tuwakaribishe waishi nchini mwetu na kufanya biashara, kwa sababu tunayo nchi ya kututosha sisi na wao pia; kisha tutaoa binti zao na kuwaoza binti zetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu hawa wanataka kukaa kwetu katika nchi yetu na kutengemana, wachuuzie huku; nanyi mnaiona nchi hii kuwa pana huku na huko, waenee nao; wana wao wa kike tutajichukulia kuwa wake zetu, nao wana wetu wa kike tutawapa wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu hawa wana amani nasi, basi na wakae katika nchi, na kufanya biashara humo; kwa maana nchi ni kubwa, yawatosha; na tuwatwae binti zao kuwa wake zetu, na binti zetu tuwape wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Watu hawa ni warafiki zetu. Tuwakaribishe waishi katika inchi yetu na kufanya biashara, kwa sababu tuko na inchi ya kututosha sisi na wao vilevile; kisha tutaoa wabinti zao na kuwaoshea binti wetu.