Genesis 34:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku tatu baadaye, waliotahiriwa wakiwa bado wana maumivu makali, watoto wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, kaka zake Dina, walizitwaa panga zao, wakauvamia mji ghafla na kuwaua wanaume wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya siku tatu, wakati wote wakiwa wangali katika maumivu, wana wawili wa Yakobo, yaani Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua panga zao na kuvamia mji ambao haukutazamia vita, wakaua kila mwanaume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua waume wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku tatu baadaye, waliotahiriwa wakiwa bado wana maumivu makali, watoto wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, kaka zake Dina, walizitwaa panga zao, wakauvamia mji ghafla na kuwaua wanaume wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya siku tatu, wakati wote wakiwa wangali katika maumivu, wana wawili wa Yakobo, yaani Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua panga zao nakuvamia mji ambao haukutazamia vita, wakaua kila mwanaume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya siku tatu, wakati wote wakiwa wangali katika maumivu, wana wawili wa Yakobo, yaani Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua panga zao na kuvamia mji ambao haukutazamia vita, wakaua kila mwanaume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua wanaume wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku tatu baadaye, waliotahiriwa wakiwa bado wana maumivu makali, watoto wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, kaka zake Dina, walizitwaa panga zao, wakauvamia mji ghafla na kuwaua wanaume wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wanaumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua kila mtu upanga wake, wakaingia mle mjini, watu walimokaa na kutulia, wakawaua wa kiume wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua waume wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha siku tatu, waliotahiriwa wakiwa wangali na maumivu makali, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, kaka za Dina, wakatwaa panga zao, wakashambulia muji kwa rafla na kuwaua wanaume wote.