Genesis 34:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya mauaji hayo, watoto wengine wa kiume wa Yakobo waliingia mjini na kuuteka nyara mji huo, kwa sababu dada yao alikuwa amenajisiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wana hao wengine wa Yakobo wakaingia mji uliojaa maiti na kuteka nyara katika mji huo dada yao alikuwa amenajisiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya mauaji hayo, watoto wengine wa kiume wa Yakobo waliingia mjini na kuuteka nyara mji huo, kwa sababu dada yao alikuwa amenajisiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wana wa Yakobo walipita juu ya maiti katika kuteka nyara mji ule ambamo dada yao alikuwa amenajisiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wana wa Yakobo walipita juu ya maiti katika kuteka nyara mji ule ambamo dada yao alikuwa amenajisiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Yakobo wakawajia hao waliouawa, wakaupora mji kwa sababu wamemharibu dada yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya mauaji hayo, watoto wengine wa kiume wa Yakobo waliingia mjini na kuuteka nyara mji huo, kwa sababu dada yao alikuwa amenajisiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wana wengine wa Yakobo walipowajia wale waliouawa, wakaziteka mali za humo mjini, kwa kuwa walimchafua umbu lao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya mauaji hayo, wana wengine wa Yakobo wakaingia katika muji na kunyanganya mali yote katika muji ule, kwa sababu dada yao alikuwa amechafuliwa.