Genesis 34:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliteka nyara mali yote, watoto na wanawake wote na chochote kilichokuwa majumbani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliteka utajiri wao wote, pamoja na wanawake na watoto wao, wakapora kila kitu ndani ya nyumba zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliteka nyara mali yote, watoto na wanawake wote na chochote kilichokuwa majumbani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walichukua utajiri wao wote pamoja na wanawake na watoto wao, wakachukua nyara kila kitu ndani ya nyumba zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walichukua utajiri wao wote pamoja na wanawake na watoto wao, wakachukua nyara kila kitu ndani ya nyumba zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakatwaa na mali zao zote, watoto wao wote, na wake zao wakateka na hata wakapora vyote vilivyokuwemo nyumbani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliteka nyara mali yote, watoto na wanawake wote na chochote kilichokuwa majumbani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakateka mali zao zote na wana wao wote na wake zao, nayo yote yaliyokuwamo nyumbani wakayanyang'anya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walitwaa mali yote, watoto na wanawake wote na chochote kilichokuwa ndani ya nyumba zao.