Genesis 34:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yakobo akapata habari kwamba Dina, bintiye, alikuwa amenajisiwa na Shekemu; lakini kwa kuwa wanawe walikuwa malishoni, alinyamaza mpaka waliporudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake. Kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo hadi waliporudi nyumbani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yakobo akapata habari kwamba Dina, bintiye, alikuwa amenajisiwa na Shekemu; lakini kwa kuwa wanawe walikuwa malishoni, alinyamaza mpaka waliporudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake, kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo mpaka waliporudi nyumbani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake, kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo mpaka waliporudi nyumbani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hadi walipokuja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yakobo akapata habari kwamba Dina, bintiye, alikuwa amenajisiwa na Shekemu; lakini kwa kuwa wanawe walikuwa malishoni, alinyamaza mpaka waliporudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yakobo aliposikia, ya kuwa yule amemchafua mwanawe Dina, wanawe waume walikuwa porini pamoja na makundi yake, kwa hiyo Yakobo akanyamaza kimya, mpaka wakirudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yakobo akapata habari kwamba Sekemu amemuchafua binti yake Dina; lakini kwa sababu wana wake walikuwa pamoja na nyama kwenye malisho, akanyamaza mpaka waliporudi.