Genesis 35:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu mwenye nguvu. Ujaliwe wazawa wengi; kwako wewe kutatokea taifa, mataifa na wafalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu mwenye nguvu. Ujaliwe wazawa wengi; kwako wewe kutatokea taifa, mataifa na wafalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi, ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka katika uzao wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu mwenye nguvu. Ujaliwe wazawa wengi; kwako wewe kutatokea taifa, mataifa na wafalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mungu akamwambia: Mimi ni Mungu Mwenyezi; na uzae wana, upate kuwa wengi, taifa na kundi zima la mataifa litatoka kwako, nao wafalme watatoka kiunoni mwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena Mungu akamwambia: “Mimi ni Mungu Mwenye Nguvu. Ujaliwe wazao wengi na kuongezeka. Taifa na kundi la mataifa watatokea kwako na wafalme watatokea katika uzao wako.