Genesis 35:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yakobo na jamaa yake yote waliendelea na safari yao kutoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efratha, Raheli akashikwa na uchungu mkali wa kuzaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wakaondoka Betheli. Kabla hawajafika Efrata, Raheli akaanza kujifungua na akapata shida kuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yakobo na jamaa yake yote waliendelea na safari yao kutoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efratha, Raheli akashikwa na uchungu mkali wa kuzaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasafiri kutoka Betheli, na kabla ya kufika Efrata, Raheli akashikwa na uchungu wa kuzaa, na uchungu wake ulikuwa mkali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yakobo na jamaa yake yote waliendelea na safari yao kutoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efratha, Raheli akashikwa na uchungu mkali wa kuzaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakaondoka Beteli. Ikawa, uliposalia mwendo wa kipande kifupi tu kufika Efurata, Raheli akazaa, nako huko kuzaa kwake kukawa kugumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yakobo na jamaa yake yote wakaendelea na safari yao kutoka Beteli. Walipokuwa umbali fulani mbele ya kufika Efurata, Rakeli akashikwa na uchungu mukali wa kuzaa.