Genesis 36:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike, watu wote wa nyumbani mwake, ng'ombe wake, wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata katika nchi ya Kanaani, akahamia mahali pengine, mbali na nduguye Yakobo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike, na watu wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote, na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike, watu wote wa nyumbani mwake, ng'ombe wake, wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata katika nchi ya Kanaani, akahamia mahali pengine, mbali na nduguye Yakobo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoipata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike, watu wote wa nyumbani mwake, ng'ombe wake, wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata katika nchi ya Kanaani, akahamia mahali pengine, mbali na nduguye Yakobo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Esau akawachukua wakeze na wanawe wa kiume na wa kike nao wote waliokuwa nyumbani mwake na mbuzi na kondoo wake na nyama wengine wote, aliowafuga, na mapato yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani, akaondoka kwa ndugu yake Yakobo, akaenda katika nchi nyingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng’ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Esau akawatwaa wake zake, watoto wake wanaume na wanawake, watu wote wa nyumba yake, ngombe wake, nyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata katika inchi ya Kanana, akahamia pahali pengine, mbali na ndugu yake Yakobo.