Genesis 36:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alifanya hivyo kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi hata wasiweze kuishi pamoja. Nchi waliyokaa kama wageni haikuweza kuwatosha kwa sababu ya wingi wa mifugo yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mali yao ilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja; nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alifanya hivyo kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi hata wasiweze kuishi pamoja. Nchi waliyokaa kama wageni haikuweza kuwatosha kwa sababu ya wingi wa mifugo yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mali yao ilikuwa nyingi wasiweze kukaa pamoja, wala nchi ya ugeni haikuweza kuwapokea kwa sababu ya wingi wa mifugo wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alifanya hivyo kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi hata wasiweze kuishi pamoja. Nchi waliyokaa kama wageni haikuweza kuwatosha kwa sababu ya wingi wa mifugo yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mapato yao yalikuwa mengi, wasiweze kukaa pamoja; nayo nchi hiyo, waliyoikaa ugeni, haikuweza kuwaeneza kwa ajili ya makundi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alifanya hivyo kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi hata wasiweze kuishi pamoja. Inchi walimokaa kama wageni haikuweza kuwatoshelea kwa sababu ya wingi wa nyama wao.