Genesis 37:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini alipomsimulia baba yake na ndugu zake ndoto hiyo, baba yake alimkemea akisema, “Ni ndoto gani hiyo uliyoota? Je, itatulazimu mimi, mama yako na ndugu zako kuja kuinama chini kwa heshima mbele yako?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako, na mimi, na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini alipomsimulia baba yake na ndugu zake ndoto hiyo, baba yake alimkemea akisema, “Ni ndoto gani hiyo uliyoota? Je, itatulazimu mimi, mama yako na ndugu zako kuja kuinama chini kwa heshima mbele yako?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako na mimi na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe hadi nchi?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako na mimi na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe hadi nchi?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie mpaka chini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini alipomsimulia baba yake na ndugu zake ndoto hiyo, baba yake alimkemea akisema, “Ni ndoto gani hiyo uliyoota? Je, itatulazimu mimi, mama yako na ndugu zako kuja kuinama chini kwa heshima mbele yako?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipomsimulia baba yake nao kaka zake ndoto hizi, baba yake akamkemea, akamwambia: Hiyo ndoto yako, uliyoiota, ni ndoto gani? Je? mimi na mama yako na kaka zako tuje, tukuangukie chini?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini alipomwelezea baba yake na wandugu zake ndoto hiyo, baba yake alimukaripia, akisema: “Ni ndoto gani hiyo uliyoota? Itatupasa mimi, mama yako na wandugu zako kuja kuinama chini kwa heshima mbele yako?”