Genesis 37:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafanyabiashara Wamidiani walipofika mahali hapo, hao ndugu wakamtoa Yosefu katika shimo, wakamwuza kwa Waishmaeli kwa bei ya vipande ishirini vya fedha; nao wakamchukua Yosefu hadi Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yusufu kutoka lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafanyabiashara Wamidiani walipofika mahali hapo, hao ndugu wakamtoa Yosefu katika shimo, wakamwuza kwa Waishmaeli kwa bei ya vipande ishirini vya fedha; nao wakamchukua Yosefu hadi Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo na kumwuza kwa shekeli ishirini za fedha kwa wale Waishimaeli, ambao walimpeleka Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yusufu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika shimo, wakamuuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafanyabiashara Wamidiani walipofika mahali hapo, hao ndugu wakamtoa Yosefu katika shimo, wakamwuza kwa Waishmaeli kwa bei ya vipande ishirini vya fedha; nao wakamchukua Yosefu hadi Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, hao wachuuzi wa Midiani walipopita, wakamwopoa Yosefu na kumtoa mle shimoni, wakamwuza Yosefu kwao hao Waisimaeli kwa fedha 20, nao wakampeleka Yosefu Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wachuuzi Wamidiani walipofika pahali pale, wale wandugu wakamwondoa Yosefu katika shimo, wakamwuzisha kwa Waisimaeli kwa bei ya vikoroti makumi mbili vya feza; nao wakamupeleka Yosefu Misri.