Genesis 37:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baba yao akaitambua hiyo kanzu, akasema, “Ndiyo hasa! Bila shaka mnyama wa porini amemshambulia na kumla. Hakika Yosefu ameraruliwa vipandevipande.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba yao akalitambua, akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yusufu ameraruliwa vipande vipande.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baba yao akaitambua hiyo kanzu, akasema, “Ndiyo hasa! Bila shaka mnyama wa porini amemshambulia na kumla. Hakika Yosefu ameraruliwa vipandevipande.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yusufu ameraruliwa vipande vipande.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baba yao akaitambua hiyo kanzu, akasema, “Ndiyo hasa! Bila shaka mnyama wa porini amemshambulia na kumla. Hakika Yosefu ameraruliwa vipandevipande.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaitambua, akasema: Ni kanzu ya mwanangu! Nyama mkali amemla, Yosefu ameraruliwa kweli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Baba yao akatambua hiyo kanzu, akasema: “Ndiyo ni kanzu ya mwana wangu! Bila shaka nyama wa pori amemushambulia na kumukula. Hakika Yosefu ameraruliwa vipandevipande.”