Genesis 37:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watoto wake wa kiume na wa kike wakamjia ili kumfariji, lakini akakataa kufarijiwa, akisema, “Niacheni; nitaendelea kuomboleza kwa ajili ya mwanangu, mpaka nitakaposhuka kuzimu alipo.” Ndivyo baba yake alivyomlilia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanawe wote wa kiume na wa kike wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu hadi nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watoto wake wa kiume na wa kike wakamjia ili kumfariji, lakini akakataa kufarijiwa, akisema, “Niacheni; nitaendelea kuomboleza kwa ajili ya mwanangu, mpaka nitakaposhuka kuzimu alipo.” Ndivyo baba yake alivyomlilia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanawe wote na binti zake wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu mpaka nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanawe wote na binti zake wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu mpaka nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitashuka kaburini kwa mwanangu, nikiomboleza. Basi baba yake akamlilia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watoto wake wa kiume na wa kike wakamjia ili kumfariji, lakini akakataa kufarijiwa, akisema, “Niacheni; nitaendelea kuomboleza kwa ajili ya mwanangu, mpaka nitakaposhuka kuzimu alipo.” Ndivyo baba yake alivyomlilia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakainuka wanawe wote wa kiume nao wote wa kike, wamtulize moyo, lakini akakataa kutulizwa moyo akisema: Nitashuka mwenye ukiwa huko kuzimuni, mwanangu aliko. Ndivyo, baba yake alivyomlilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watoto wake wanaume na wanawake wakamufikia kwa kumufariji, lakini akakataa kufarijiwa, akisema: “Uniache. Nitaendelea kuomboleza kwa ajili ya mwana wangu, mpaka nitakaposhuka katika kaburi.” Ndivyo baba yake alivyomulilia.