Genesis 38:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
alivua mavazi yake ya ujane na kujifunika shela kisha akaketi penye lango la kuingilia Enaimu, kijiji kilichokuwa njiani kwenda Timna. Alifanya hivyo kwa vile aliona kwamba Shela alikwisha kuwa mtu mzima, lakini yeye Tamari hakuozwa awe mkewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike. Akaketi kwenye mlango wa Enaimu, njiani ya kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba ingawa Shela sasa alikuwa mtu mzima, bado hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
alivua mavazi yake ya ujane na kujifunika shela kisha akaketi penye lango la kuingilia Enaimu, kijiji kilichokuwa njiani kwenda Timna. Alifanya hivyo kwa vile aliona kwamba Shela alikwisha kuwa mtu mzima, lakini yeye Tamari hakuozwa awe mkewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, ijapokuwa hakuozwa awe mkewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
alivua mavazi yake ya ujane na kujifunika shela kisha akaketi penye lango la kuingilia Enaimu, kijiji kilichokuwa njiani kwenda Timna. Alifanya hivyo kwa vile aliona kwamba Shela alikwisha kuwa mtu mzima, lakini yeye Tamari hakuozwa awe mkewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akayavua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa ukaya na kujitandia nguo, kisha akakaa hapo pa kuingilia Enaimu kwenye njia ya timunati, kwani aliona, ya kuwa Sela amekwisha kukua, lakini yeye hakuozwa naye, awe mkewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akavua nguo zake za ujane na kujifunika kitambaa. Kisha akaikaa kwenye mulango wa kuingilia Enaimu, kijiji kilichokuwa katika njia kwenda Timuna. Alifanya hivyo kwa vile aliona kwamba Sela alikwisha kuwa mutu muzima, lakini yeye Tamari hakuoeshwa akuwe muke wake.