Genesis 38:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yuda akamjibu, “Nitakupa mwanambuzi kutoka kundi langu.” Tamari akamwambia, “Weka rehani kuthibitisha utaniletea huyo mwanambuzi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.” Akamuuliza, “Utanipa amana hadi utakapompeleka?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Nitakuletea mwana-mbuzi wa kundini. Naye akamwuliza, Je! Utanipa rehani hata utakapomleta?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yuda akamjibu, “Nitakupa mwanambuzi kutoka kundi langu.” Tamari akamwambia, “Weka rehani kuthibitisha utaniletea huyo mwanambuzi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.” Akamwuliza, “Utanipa kitu cho chote kama amana mpaka utakapompeleka?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.” Akamuuliza, “Utanipa kitu chochote kama amana mpaka utakapompeleka?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nitakuletea mwana-mbuzi kutoka kundini. Naye akamwuliza, Je! Utanipa rehani hata utakapomleta?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yuda akamjibu, “Nitakupa mwanambuzi kutoka kundi langu.” Tamari akamwambia, “Weka rehani kuthibitisha utaniletea huyo mwanambuzi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Mimi nitakuletea dume la mbuzi, nitakayemtoa mle makundini; naye akamwambia: Nipe rehani, niishike, mpaka utakapomleta!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Nitakuletea mwana-mbuzi wa kundini. Naye akamwuliza, Je! Utanipa rehani hata utakapomleta?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yuda akamujibu: “Nitakupa mwana-mbuzi kutoka kundi langu.” Tamari akamwambia: “Weka rehani kwa kuhakikisha kwamba utaniletea yule mwana-mbuzi.”